Ecclesiastes 5:13-19

13 aNimeshaona uovu mzito chini ya jua:

Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima
na kuleta madhara kwa mwenye mali,
14au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya,
hivyo kwamba wakati akiwa na mwana
hakuna chochote kilichobaki kwa ajili yake.
15 bMtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi,
naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka.
Hachukui chochote kutokana na kazi yake
ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake.
16 cHili nalo ni baya la kusikitisha:

Kama vile mtu ajavyo, vivyo hivyo huondoka,
naye anapata faida gani,
maadamu hutaabika kwa ajili ya upepo?
17Siku zake zote hula gizani,
pamoja na fadhaa kubwa,
mateso na hasira.
18 dNdipo nikatambua kwamba ni vyema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake. 19 eZaidi ya yote, Mungu anapompa mtu yeyote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu.
Copyright information for SwhNEN